Saturday, 26 October 2019

KUTENGENEZA FLASH YENYE VIRUS

Tumekuwa tuna pata shida Sana pale ambapo flash zetu zinajaa virus, na kufikia wakati hazifanyi kazi na kulazimika kununua mpya. Kila unapoweka kwenye computer yako inakuandika format disk au insert disk au disk unreadable. Nini chakufanya hiki fuata hatua zifuatazo na flash yako inapona kabisa. 1. Chomeka flash kwenye computer yako Kisha nenda upande was chini kushoto Kuna kitufe Cha kusearch Kisha andika neno"CMD" na piga ok.

2. Andika neno disk part Kisha piga ok
3. Andika neno list disk na piga ok
4. Zitakuja local disk c, d pamoja na ya flash yako angalia kwa makini flash yako namba ngapi na Kisha andika neno select disk3 Kama flash yako imejipanga namba tatu labda.
5. Andika neno clean na piga ok
6. Andika create partition primary piga ok
7. Andika format file system=fat32 quick na piga ok
8. Utaona flash yako imefunguka upya.
Karibuni Tena kwa darasa lijalo

1 comment: