Sunday 27 October 2019

PAY THE PRICE FOR YOUR ARCHIVEMENT

Dunia ni kama kitabu usipotembea utaishia kusoma ukurusa mmoja tu hasa wa mbele. Ni kweli tumekuwa na jamii ya watu aina mbalimbali ambao wengi wanapenda kuletewa Mambo au vitu walipo, kusikia bila kutafiti na ndio mwishoni kugeuzwa kuwa vibaraka was wanao penda kutembea ili kutafuta fursa. Kuna wakati unaeza jikuta unajilaumu kuwa huna bahati kimbe fursa yako haiko hapo ulipo ipo kijiji Cha pili toka hapo ulipo au mkoa mwingine hata wilaya au nchi nyingine. Tumepewa uwezo wa kufikiri na Uhuru wa kufanya tupendalo japo wengi wamekua waoga wa maisha na kuogopa kujaribu fursa mbalimbali kwa kushikiria walichonacho bila kujua Kuna wakati kubwa zaidi linakungoja mbele. Maisha ni kuamua na wahenga walisema penye Nia pana njia. Tupende kutembea ili tujifunze na kuona mengi kuweza kupata wigo was fursa mbalimbali zilizo tuzunguka. LIPIA GHARAMA YA MAFANIKIO YAKO

No comments:

Post a Comment